TANGAZO LA AJIRA – HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA 2026
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA
Ref. No.: LDC/L.10/12 Vol. VI/30 | Tarehe: 31 Desemba 2025
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi nane (8) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 4
Majukumu na Kazi
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (log book).
- Kufanya usafi wa gari.
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
Sifa za Mwombaji
- Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Udereva Daraja E au C.
- Uzoefu wa kuendesha gari kwa mwaka mmoja (1) bila ajali.
- Vyeti vya mafunzo vinavyompa sifa ya kupata daraja husika.
- Halikadiri, awe amehudhuria Basic Driving Course kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Ngaazi ya Mshahara: TGS B
2.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 4
Majukumu na Kazi
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni, kusikiliza shida zao na kuwaelekeza sehemu husika.
- Kutunza taarifa za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika kwa utekelezaji wa kazi.
- Kupokea na kusambaza majalada kwa maofisa wa idara husika.
- Kukusanya, kutunza na kurejesha majalada sehemu husika.
- Kuandaa dondoo na maandalizi ya vikao mbalimbali.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
Sifa za Mwombaji
- Elimu ya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita.
- Stashahada ya Uhifadhi / NTA Level 6 katika Uhifadhi wa Ofisi.
- Uwezo wa Kiswahili na Kiingereza, 100 maneno kwa dakika moja kwa Hatimkato.
- Ujuzi wa kutumia Microsoft Word, Excel, PowerPoint, Windows, Internet, E-mail na Publisher.
Ngaazi ya Mshahara: TGS C
Masharti ya Jumla
- Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.
- Ambatanishe Cheti cha Kuzaliwa.
- Detailed CV yenye anuani, namba za simu na majina ya wadhamini.
- Vyeti vya taaluma na Kidato cha Nne/Sita pamoja na mafunzo husika, vipandikwe kwenye Ajira Portal.
- Testimonials, Provision Results, Statement of Results HAVIKUBALIKI.
- Waombaji kazi wa Dereva II lazima waambatanishe vyeti vya mafunzo ya Udereva.
- Picha mbili (2) za Passport Size za hivi karibuni.
- Vyeti vya waliosoma nje ya nchi vinapaswa kuthibitishwa na TCU, NECTA, NACTE.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waajiriwa walioko katika nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
- Uwasilishwaji wa taarifa au nyaraka za kughushi utachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi: 11 Januari 2026.
Maelekezo Muhimu
Kumbuka kuambatanisha barua ya maombi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Barua ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa,
S.L.P 19,
LUDEWA.
Muundo wa Maombi
Maombi yote yatumwe kwa njia ya kielektroniki kupitia Ajira Portal:
Maombi yasiyoendana na utaratibu huu hayatafanyiwa kazi.
Limetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA