TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA – JANUARI 2026
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi tatu (03) baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR–TAMISEMI).
NAFASI ZILIZOTANGAZWA
DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 03
MAJUKUMU NA KAZI
Mwombaji atatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali katika safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
- Kufanya usafi wa gari.
- Kufanya kazi nyingine atakazoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
- Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
- Leseni ya Udereva Daraja E au C.
- Uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali.
- Vyeti vya mafunzo vilivyompatia sifa ya kupata daraja husika.
- Mafunzo ya Msingi ya Udereva (Basic Driving Course) kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
TGS B
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.
- Waambatanishe Cheti cha Kuzaliwa.
- Waambatanishe Detailed CV yenye anuani, namba za simu na majina ya wadhamini (Referees).
- Waweke nakala za vyeti vya taaluma, Kidato cha Nne na Sita pamoja na vyeti vya mafunzo kupitia Ajira Portal.
- Testimonials, Provision Results na Statement of Results HAVIKUBALIKI.
- Waombaji wa Dereva II wenye Leseni E au C lazima waambatanishe vyeti vya mafunzo ya udereva.
- Waweke picha mbili (2) za Passport Size za hivi karibuni kwenye Ajira Portal.
- Waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTE.
- Waliofukuzwa au kustaafishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waajiriwa wa Serikali katika nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba kwa mujibu wa Waraka wa 30 Novemba 2010.
- Kughushi taarifa au nyaraka kutachukuliwa hatua za kisheria.
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 13 Januari, 2026.
MAELEKEZO MUHIMU
Waombaji waambatanishe barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu.
Barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
S.L.P. 160
KILWA
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya kielektroniki kupitia Mfumo wa Ajira (Recruitment Portal)
kupitia anuani ifuatayo:
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliobainishwa katika tangazo hili hayatafanyiwa kazi.