Muhtasari wa Mwongozo wa Kujitolea katika Utumishi wa Umma Tanzania (PDF)

MUHTASARI WA MWONGOZO WA KUJITOLEA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa Mwongozo wa Kujitolea katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kuweka utaratibu wa kitaifa wa kusimamia vijana wanaojitolea katika Taasisi za Umma.

Mwongozo huu unalenga kuhakikisha uwazi, usawa, ufanisi na ulinzi wa haki za vijana wa kujitolea sambamba na kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.

Changamoto Zilizokuwepo Awali

  • Kukosekana kwa utaratibu wa pamoja wa kuwapata vijana wa kujitolea
  • Muda wa kujitolea kutokua bayana
  • Ukosefu wa usimamizi wa utendaji kazi
  • Kutotolewa kwa vyeti vya uhitimu
  • Kushuka kwa ari ya kujitolea miongoni mwa vijana

Yaliyomo Kwenye Mwongozo

  • Sifa za vijana wa kujitolea
  • Utaratibu wa wazi wa kuwapata vijana
  • Muda wa kujitolea usiozidi miezi 12
  • Haki na wajibu wa vijana wa kujitolea
  • Maadili, nidhamu na usimamizi wa kazi
  • Mafunzo, ufuatiliaji na tathmini ya utendaji kazi

Hitimisho

Mwongozo huu unalenga kuwawezesha vijana kupata ujuzi na uzoefu wa kazi, kukuza uzalendo na kuongeza tija katika Utumishi wa Umma, bila kuifanya kujitolea kuwa njia ya moja kwa moja ya ajira.

PDF Icon DOWNLOAD PDF FILE
Previous Post Next Post

نموذج الاتصال