SMART EDUCATION TANZANIA
Muongozo wa Kubadilisha Masomo na Vyuo kupitia SELFORM System
Utangulizi
Mfumo wa SELFORM unawawezesha wahitimu wa kidato cha nne kubadilisha taarifa zao, ikiwemo masomo, vyuo na machaguo ya kidato cha tano au vyuo vya kati kulingana na matokeo yao ya mtihani.
Walengwa wa Mfumo Huu
- Wahitimu wa Kidato cha Nne
- Wanafunzi wanaobadilisha mchepuo wa Kidato cha Tano
- Waombaji wa Vyuo vya Kati (Middle Level Colleges)
Jinsi ya Kuingia SELFORM
- Unganisha kifaa chako na mtandao wa intaneti.
- Fungua browser kama Chrome.
- Nenda: https://selform.tamisemi.go.tz
Usajili wa Mara ya Kwanza
- Bofya “For Candidates, Click here to Register”.
- Weka namba ya mtihani (mfano: S0101.0020.2018).
- Weka jina la ukoo na mwaka wa kuzaliwa.
- Jibu swali la usalama (security question).
Kuweka Nenosiri (Password)
Tengeneza password yako ya kipekee itakayotumika kila mara kuingia kwenye mfumo. Hakikisha unaikumbuka vizuri kwa matumizi ya baadaye.
Kubadilisha Machaguo au Chuo
- Ingia kwenye akaunti yako.
- Fungua sehemu ya “Choices Selection”.
- Chagua mchepuo au chuo kipya unachotaka.
- Hifadhi mabadiliko (Save Changes).
Pakua Mwongozo Kamili
Hitimisho
Fuata hatua hizi kwa umakini ili kuhakikisha mabadiliko yako yanakubaliwa kikamilifu kwenye mfumo wa SELFORM. Endelea kufuatilia Smart Education Tanzania kwa taarifa zaidi za elimu na miongozo muhimu.

Tafadhali Tuambie kupitia hapa