Tazama Majina ya Walioitwa JKT 2026/2027 – Jinsi ya Kuangalia na Maelekezo Muhimu

Mr.Izow
0

Majina ya Walioitwa JKT 2026/2027 – Jinsi ya Kuangalia na Maelekezo Muhimu

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza rasmi majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mwaka 2026/2027.


📌 Jinsi ya Kuangalia Jina Lako

Orodha rasmi za waliochaguliwa zimepangwa kulingana na shule walizosoma wanafunzi husika. Ili kuangalia jina lako, fuata hatua hizi:

  1. Tembelea tovuti rasmi ya JKT kupitia www.jkt.go.tz
  2. Tafuta tangazo lenye kichwa: “Selection of Form Six Graduates for National Service 2026”
  3. Pakua faili la PDF lenye majina ya walioitwa.
  4. Tumia sehemu ya kutafuta (Ctrl + F) kuandika jina lako au jina la shule yako.

📅 Taarifa Muhimu za Kuripoti

Wanafunzi wote waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti katika makambi waliopangiwa ndani ya tarehe zilizotangazwa rasmi.

Kutofika kambini bila sababu maalum inayotambulika kisheria kunaweza kuchukuliwa kama kosa kwa mujibu wa sheria za nchi.


📄 Nyaraka Muhimu za Kuambatana Nazo

Unatakiwa kuwa na nyaraka halisi zifuatazo wakati wa kuripoti:

  • Cheti cha kuzaliwa
  • Cheti au Result Slip ya Kidato cha Nne
  • Result Slip au Cheti cha Kidato cha Sita
  • Namba ya NIDA au Kitambulisho cha Taifa

🎒 Vifaa Muhimu vya Kwenda Navyo

Ingawa serikali itatoa baadhi ya mahitaji ya msingi, kila mwanafunzi anatakiwa kwenda na vifaa vifuatavyo:

  • Suruali fupi mbili za blue
  • Raba nyeupe za michezo
  • Tracksuit ya blue au green
  • Mashuka ya light blue
  • Chandarua cha mviringo cha rangi nyeupe au green
  • Sahani ya chuma, kikombe na kijiko
  • Fomu ya uchunguzi wa afya kutoka hospitali ya serikali

🏕️ Baadhi ya Makambi ya JKT Tanzania

  • JKT Rwamkoma – Mara
  • JKT Msange – Tabora
  • JKT Ruvu & Kibiti – Pwani
  • JKT Mpwapwa & Makutupora – Dodoma
  • JKT Mafinga – Iringa
  • JKT Mlale – Ruvuma
  • JKT Mgambo & Maramba – Tanga
  • JKT Makuyuni & Orjolo – Arusha
  • JKT Bulombora, Kanembwa & Mtabila – Kigoma
  • JKT Itaka – Songwe
  • JKT Luwa & Milundikwa – Rukwa
  • JKT Nachingwea – Lindi

⚠️ Muhimu kwa Wahitimu

Hakikisha unasoma maelekezo maalum ya kambi uliyopangiwa kwani baadhi ya makambi yanaweza kuwa na mahitaji tofauti kidogo.

Ikiwa tovuti rasmi ya JKT itakuwa nzito kutokana na watu wengi kuingia kwa wakati mmoja, subiri kwa muda na ujaribu tena baadaye.


Imetolewa na SMART EDUCATION TANZANIA

Chapisha Maoni

0 Maoni

Tafadhali Tuambie kupitia hapa

Chapisha Maoni (0)
3/related/default