Mwongozo wa Udahili wa NACTVET 2026/2027 kwa Kozi za Certificate na Diploma
NACTVET imetoa rasmi Guidebook ya Udahili kwa mwaka wa masomo 2026/2027 kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vya ufundi na elimu ya kati nchini Tanzania.
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limetoa mwongozo rasmi wa udahili kwa kozi za Certificate na Diploma zinazotolewa katika taasisi mbalimbali za elimu ya ufundi nchini Tanzania kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
Mwongozo huu unawasaidia wanafunzi kupata taarifa muhimu kuhusu kozi zinazopatikana, sifa za kujiunga, ada za masomo, muda wa kozi pamoja na vyuo vinavyotoa programu hizo.
Yaliyomo Kwenye Mwongozo wa Udahili wa NACTVET 2026/2027
Guidebook ya NACTVET ina taarifa muhimu zifuatazo:
- Orodha ya vyuo vya ufundi vilivyosajiliwa Tanzania
- Kozi za Certificate na Diploma zinazotolewa
- Sifa za chini za kujiunga kwa kila kozi
- Ada za masomo na muda wa programu
- Aina ya umiliki wa chuo (Serikali, binafsi au taasisi za dini)
- Idadi ya wanafunzi wanaopokelewa kwa kila chuo
- Taratibu za kufanya maombi ya udahili
Kwa mujibu wa NACTVET, programu zimegawanywa katika makundi mbalimbali ikiwemo:
- Health and Allied Sciences (HAS)
- Science and Allied Technologies (SAT)
- Business, Tourism and Planning (BTP)
Mwongozo huo pia unaonesha programu za NTA Level 4, NTA Level 5 na NTA Level 6.
Sifa za Kujiunga na Kozi za Certificate na Diploma
NACTVET imeeleza kuwa waombaji wa kozi za Certificate na Diploma wanapaswa kuwa na angalau ufaulu wa masomo manne yasiyo ya dini katika mtihani wa kidato cha nne (CSEE).
Baadhi ya kozi zinaweza kuhitaji masomo maalum kulingana na fani husika.
Kwa mfano:
- Kozi za afya kama Nursing, Clinical Medicine na Pharmaceutical Sciences huhitaji ufaulu wa Biology, Chemistry na Physics.
- Kozi za Engineering na ICT mara nyingi huhitaji Mathematics na Physics.
Umuhimu wa Guidebook ya NACTVET
Mwongozo huu huwasaidia wanafunzi:
- Kutambua vyuo vilivyosajiliwa rasmi
- Kulinganisha ada za vyuo mbalimbali
- Kuelewa sifa za kujiunga na kozi
- Kuchagua kozi kulingana na malengo yao ya taaluma
- Kuepuka kuomba katika vyuo visivyosajiliwa
Waombaji wanashauriwa kusoma guidebook kwa umakini kabla ya kutuma maombi yao ya udahili.
Jinsi ya Kufanya Maombi ya Udahili Kupitia NACTVET
Wanafunzi wanapaswa kufanya maombi moja kwa moja katika vyuo vinavyotoa kozi zilizoorodheshwa kwenye guidebook.
Udahili hufuata kalenda rasmi ya NACTVET pamoja na dirisha la maombi linalotangazwa rasmi.
Waombaji wanapaswa kuandaa nyaraka zifuatazo:
- Vyeti vya masomo na transcripts
- Cheti cha kuzaliwa
- Picha za passport size
- Nyaraka za utambulisho
- Ada ya maombi pale inapohitajika
Download Guidebook ya NACTVET 2026/2027
Wanafunzi wanaweza kupakua guidebook rasmi ya NACTVET kupitia link hapo chini:
Kuhusu NACTVET
NACTVET ni baraza linalosimamia na kuratibu elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania. Baraza hili lina jukumu la kuhakikisha ubora wa elimu, usajili wa taasisi pamoja na usimamizi wa udahili katika vyuo vya ufundi.
Kwa taarifa zaidi kuhusu elimu, udahili, guidebook, selection na scholarship mbalimbali, tembelea Smart Education Tanzania.


Tafadhali Tuambie kupitia hapa