🔔 TANGAZO MUHIMU
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI 2026
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Tume ya Madini (TMC), National Housing Corporation (NHC) na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba nafasi mbalimbali kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 20/01/2026 hadi 14/02/2026.
📌 Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
- Usaili utafanyika kwa tarehe, muda na sehemu zilizoainishwa kwa kila Kada.
- Kila msailiwa afike eneo la usaili akiwa amevaa barakoa (Mask).
- Msailiwa awe na kitambulisho halali cha utambulisho.
- Vitambulisho vinavyokubalika ni: Kitambulisho cha Taifa, Mpiga Kura, Kazi, Uraia, Pasipoti, Leseni ya Udereva au Barua ya Serikali ya Mtaa/Kijiji.
- Wasailiwa wafike na vyeti halisi kuanzia Cheti cha Kuzaliwa hadi kiwango cha juu cha elimu.
- Testimonials, Provisional Results au Statement of Results HAVITAKUBALIWA.
- Kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma zije na vyeti halisi pamoja na leseni.
- Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi.
- Waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na mamlaka husika (TCU, NACTVET au NECTA).
- Wasioona majina yao waingie kwenye akaunti zao za Ajira Portal kuona sababu.
- Wasailiwa wanapaswa kunakili namba ya usaili kutoka Ajira Portal.
- Tofauti ya majina kwenye nyaraka ihakikishwe kwa Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll).
Chanzo: Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
