TANGAZO LA KUITWA KAZINI TAREHE 20/01/2026

TANGAZO LA KUITWA KAZINI TAREHE 20/01/2026

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 18 Januari 2025 na 22 Desemba 2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.

Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye Kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Maelekezo Muhimu kwa Waliofaulu

  • Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi watapata barua za kupangiwa vituo vya kazi kupitia Akaunti zao za Ajira Portal katika sehemu ya My Applications.
  • Waombaji wanatakiwa kupakua (Download) na kuchapisha (Print) barua hizo na kwenda nazo kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa.

Maelekezo ya Kuripoti Kazini

Waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti kwa mwajiri katika muda uliobainishwa kwenye barua zao wakiwa na:

  • Vyeti halisi vya masomo (Original Certificates)
  • Kuanzia Kidato cha Nne na kuendelea
  • Kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupewa barua ya Ajira

Kwa waombaji kazi ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata nafasi au hawakufaulu usaili. Waombaji hao wanahimizwa kuendelea kuomba tena nafasi za kazi zitakapotangazwa.


Endelea kutembelea tovuti yetu kwa taarifa mpya za ajira, usaili na matokeo kutoka Sekretarieti ya Ajira.

Smart Education Tanzania

Tangazo la kuitwa kazini 2026, Majina ya waliofaulu usaili Sekretarieti ya Ajira, Ajira Portal Tanzania, Public Service Recruitment Tanzania, Kuitwa kazini Januari 2026, Matokeo ya usaili Ajira

Post a Comment

Tafadhali Tuambie kupitia hapa

Previous Post Next Post

Featured Post

Smart Education Tanzania