TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI 2026
Kupitia Mradi wa GPE – TSP | OWM – TAMISEMI
Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM – TAMISEMI), kupitia Mradi wa Kuboresha Kada ya Ualimu Global Partnership for Education – Teacher Support Programme (GPE – TSP), inatekeleza afua mbalimbali ikiwemo kuratibu upatikanaji wa Walimu wa Kujitolea katika shule za sekondari zenye uhitaji mkubwa wa walimu.
Kupitia mradi huu, OWM – TAMISEMI inatangaza nafasi 1,500 za Walimu wa Kujitolea kwa shule za sekondari zilizo chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Secondary Teacher Allocation Protocol (S – TAP).
Masomo Yanayohitajika
- Sayansi na Teknolojia (STEM)
- Masomo ya Amali (Vocational Subjects)
- Masomo ya Biashara (Business Studies)
Majukumu ya Jumla ya Mwalimu wa Kujitolea
- Kuandaa maandalio ya masomo, mipango ya kazi na nyaraka za kitaaluma
- Kutengeneza na kutumia zana za kufundishia na kujifunzia
- Kufundisha, kufanya tathmini na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi
- Kusimamia mahudhurio ya wanafunzi shuleni na darasani
- Kutoa ushauri nasaha na kusimamia malezi ya wanafunzi
- Kusimamia vifaa na mali za shule
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule
Sifa za Waombaji kwa Masomo
Fizikia (Physics) – Nafasi 504
- Shahada ya Elimu/Ualimu yenye Fizikia; au
- Shahada isiyo ya Ualimu yenye Fizikia pamoja na PGDE; au
- Stashahada ya Ualimu yenye Fizikia
Kemia (Chemistry) – Nafasi 246
- Shahada ya Elimu/Ualimu yenye Kemia; au
- Shahada isiyo ya Ualimu yenye Kemia pamoja na PGDE; au
- Stashahada ya Ualimu yenye Kemia
Biolojia (Biology) – Nafasi 332
- Shahada ya Elimu/Ualimu yenye Biolojia; au
- Shahada isiyo ya Ualimu yenye Biolojia pamoja na PGDE; au
- Stashahada ya Ualimu yenye Biolojia
Hisabati (Mathematics) – Nafasi 418
- Shahada ya Elimu/Ualimu yenye Hisabati; au
- Shahada isiyo ya Ualimu yenye Hisabati pamoja na PGDE; au
- Stashahada ya Ualimu yenye Hisabati
Masharti ya Jumla ya Waombaji
- Awe raia wa Tanzania mwenye NIDA na umri usiozidi miaka 43
- Aambatishe vyeti vya elimu, taaluma na cheti cha kuzaliwa
- Awe tayari kufanya kazi katika shule zenye uhitaji mkubwa wa walimu
- Asiwe mwajiriwa wa Serikali au taasisi nyingine
- Waombaji waliosoma nje ya nchi wawe na Equivalent Number (EQ) kutoka NECTA
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wote wenye sifa watembelee tovuti ya OWM – TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz kuanzia tarehe 01 hadi 14 Januari, 2026.
Mwisho wa kupokea maombi: 14 Januari, 2026 saa 05:59 usiku