Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Yatangazwa Rasmi na NECTA
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2025 uliofanyika kuanzia Novemba 17, 2025 katika vituo mbalimbali nchini.
Matokeo hayo yametangazwa leo, Jumamosi Januari 31, 2026, na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Profesa Said Mohammed.
Tazama Matokeo ya Kidato cha Nne 2025
Takwimu Muhimu za Mtihani wa Kidato cha Nne 2025
Kwa mujibu wa NECTA, jumla ya watahiniwa 569,883 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari, wakiwa wamesajiliwa katika shule 5,864 kote nchini. Aidha, watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 25,927 waliosajiliwa katika vituo 813.
Taarifa zinaonesha kuwa idadi ya watahiniwa wa mwaka 2025 imeongezeka kwa asilimia 7.67 ikilinganishwa na mwaka 2024.
Kati ya watahiniwa wa shule 569,914 waliosajiliwa:
- Wavulana: 266,024 sawa na asilimia 47%
- Wasichana: 303,859 sawa na asilimia 53%
Bonyeza hapa Kuangalia Matokeo ya Form Four 2025
Mahudhurio na Ufaulu
Mahudhurio ya watahiniwa katika mtihani huo yalikuwa asilimia 97.5, sawa na wanafunzi 555,606.
Ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.61 na kufikia asilimia 94.98, ambapo watahiniwa 526,620 wamefaulu kwa kupata madaraja ya I, II, III na IV.
Ufaulu wa watahiniwa waliopata daraja la kwanza hadi la tatu umefikia wanafunzi 255,404, sawa na asilimia 46.1.
NECTA imeendelea kupongeza wanafunzi, walimu na wadau wa elimu kwa mchango wao katika kuimarisha elimu nchini.
Post a Comment
Tafadhali Tuambie kupitia hapa