SOMO: MAWASILIANO YA KITAALAMU
UMAHIRI MKUU: Kumudu kuwasiliana kitaalamu UMAHIRI MAHUSUSI: Kuwasilisha taarifa za kitaaluma darasani kwa kutumia lugha stahiki SHUGHULI YA UJIFUNZAJI: Kumudu mbinu za kutoa maelekezo bayana darasani wakati wa ufundishaji na ujifunzaji
MBINU ZA UWASILISHAJI WA TAARIFA ZA KITAALUMA
a) Kutumia Zana-Uoni:
Zana hizi ni kama chati, grafu, video, modeli halisi, ubao mweupe au mweusi
Husaidia kuhusisha maudhui na maisha halisi ya wanafunzi
b) Kupangilia Uwasilishaji wa Maudhui:
Anza kwa utangulizi shirikishi
Fuata kiini kilichopangiliwa vizuri
Hitimisha kwa muhtasari wenye hoja kuu na mwito wa kuchukua hatua
c) Kutumia Mbinu Shirikishi:
Majadiliano
Vitendo
Nyimbo
Hadithi
Maswali na majibu
Kazi za vikundi
Ufundishaji kiduchu
Matumizi ya zana
d) Shughuli za Vitendo:
Huwashirikisha wanafunzi moja kwa moja katika mchakato wa ujifunzaji
e) Kutumia Teknolojia:
Programu za kompyuta za kielimu
Michezo yenye mafunzo
Hukuza uelewa wa dhana mbalimbali
f) Kutoa Mrejesho Chanya:
Huchochea ukuaji wa kitaaluma na maendeleo binafsi
Husaidia wanafunzi kutambua uwezo na udhaifu wao
Hujenga imani, uhusiano mzuri na mazingira wezeshi ya ujifunzaji
DHANA YA MAELEKEZO BAYANA
Ni mbinu ya kufundisha inayomhusisha mwalimu kuelekeza kwa uwazi na hatua kwa hatua jinsi ya kufanya jambo fulani darasani
Lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanaelewa wazi wanachopaswa kufanya, jinsi ya kufanya, na kwa nini wanapaswa kufanya hivyo
MBINU ZA KUTOA MAELEKEZO BAYANA KATIKA HATUA TATU KUU
A) Wakati wa Ufundishaji:
Tumia lugha rahisi na inayoeleweka
Eleza malengo ya somo kabla ya kuanza
Onyesha mfano wa kile kinachotarajiwa
Tumia vifaa vya kufundishia kusaidia maelekezo
Tumia mbinu shirikishi
B) Wakati wa Ujifunzaji:
Toa kazi ndogo ndogo kwa hatua
Hakikisha wanafunzi wanaelewa kila hatua
Tembea darasani kutoa msaada
Waruhusu wanafunzi kuuliza maswali
Toa mrejesho wa haraka
C) Wakati wa Upimaji:
Elekeza kwa uwazi aina ya mtihani au jaribio
Toa maelekezo ya maandishi na ya mdomo
Hakikisha maelekezo ya maswali ni wazi
Toa muda wa kutosha kwa kila sehemu
Wape wanafunzi nafasi ya kuuliza kabla ya kuanza
UMUHIMU WA MAELEKEZO BAYANA
Husaidia wanafunzi kuelewa matarajio ya kazi na somo
Huboresha ufanisi wa ujifunzaji kwa kupunguza mkanganyiko
Huongeza ushiriki wa wanafunzi
Humwezesha mwalimu kufanya tathmini kwa usahihi
MIFANO YA MBINU ZA KUTOA MAELEKEZO DARASANI
Tumia lugha sahihi na nyepesi
Toa maelekezo hatua kwa hatua
Eleza kwa vitendo kabla ya wanafunzi kufanya wenyewe
Tumia mbinu ya kupima uelewa (maswali ya kufuatilia)
Tumia zana-uoni kama michoro na chati
Tumia kauli ya kutenda (mfano: “Fanya jaribio…” badala ya “Jaribio linapaswa kufanywa…”)
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali
MASWALI YA MJADALA
Fikiria kwamba umeteuliwa kuiwakilisha shule yako katika shindano la ufundishaji. Andaa mwongozo wa mbinu utakazotumia kutoa maelekezo kwa usahihi darasani.
Eleza namna utakavyotumia mbinu za kutoa maelekezo katika kuwapima wanafunzi wako.
Ni kwa namna gani utaweza kuyafanya maelekezo changamani kueleweka kwa urahisi kwa wanafunzi wako?
Jadili ni kwa namna gani utaweza kuwahamasisha wanafunzi kuuliza maswali ikiwa hawajaelewa maelekezo.
Fafanua namna ugumu wa maelekezo unavyoweza kuathiri motisha na ujasiri wa wanafunzi katika kukamilisha kazi.
Eleza namna teknolojia inavyoweza kusaidia kuweka uwazi na ufikikaji wa maelekezo.

