banner

Mawasiliano ya Kitaaluma: Dhana, Vyanzo na Sifa Muhimu kwa Walimu

 SOMO: MAWASILIANO YA KITAALAMU


UMAHIRI MKUU: Kumudu kuwasiliana kitaalamu UMAHIRI MAHUSUSI: Kuwasilisha taarifa za kitaaluma darasani kwa kutumia lugha stahiki SHUGHULI YA UJIFUNZAJI: Kufafanua dhana ya taarifa za kitaaluma (maana, vyanzo na sifa)

MASWALI YA MWONGOZO

  1. Eleza kwa kina dhana ya taarifa za kitaaluma na umuhimu wake kwa mwalimu. (Kundi la 1 & 8)

  2. Taja na kufafanua vyanzo vitano vya taarifa za kitaaluma. (Kundi 2 & 7)

  3. Taja na eleza sifa tano za taarifa za kitaaluma na kwa nini ni muhimu kuzingatia sifa hizo. (Kundi 3 & 6)

  4. Kwa kutumia mifano, fafanua jinsi taarifa za kitaaluma zinavyotumika katika mazingira ya ualimu. (Kundi 4 & 5)

  5. Jadili changamoto tano zinazoweza kuwapata wanafunzi katika kupata au kuwasilisha taarifa za kitaaluma. (Makundi yote)

DHANA YA TAARIFA ZA KITAALUMA

  • Taarifa za kitaaluma ni vyanzo vya maarifa vinavyoandaliwa, kusambazwa na kutumika katika muktadha wa elimu.

  • Huandaliwa na wataalamu, wanazuoni na watafiti kwa ajili ya matumizi ya kielimu.

  • Husaidia kukuza maarifa, fikra tunduizi na kuchangia katika maendeleo ya taaluma husika.

  • Hupatikana katika:

    • Vitabu vya kitaaluma

    • Maandishi ya tafiti

    • Makala za majarida ya kielimu

    • Tasnifu na disertation

    • Mihadhara ya vyuoni

VYANZO VYA TAARIFA ZA KITAALUMA

A. Vyanzo vya Msingi:

  • Tafiti za awali

  • Majarida ya kisayansi

  • Mihadhara ya kitaaluma

B. Vyanzo vya Sekondari:

  • Vitabu vya kiada na rejea

  • Ripoti za kitaasisi

  • Makala za magazeti na majarida

Mfano wa vyanzo:

  • Vitabu vya kiada/ziada

  • Makala za tafiti

  • Ripoti rasmi

  • Ensaiklopidia

  • Kamusi

SIFA ZA TAARIFA ZA KITAALUMA

  1. Uhakika na uthibitisho: Zinatokana na utafiti wa kina na ushahidi wa kisayansi

  2. Marejeo ya vyanzo: Hutumia mifumo rasmi ya kunukuu kama APA

  3. Lugha rasmi ya kitaaluma: Hutumia maneno sahihi yasiyo ya kihisia

  4. Uchambuzi wa kina: Huchambua hoja kwa kutumia nadharia na ushahidi

  5. Muktadha wa kielimu: Hutolewa katika mazingira rasmi ya elimu

MASWALI YA MJADALA

  1. Kwa kutumia vyanzo vya kuaminika vya taarifa za kitaaluma, andika insha kuhusu namna uhusiano unavyoathiri maendeleo.

  2. Kwa kutumia ensaiklopidia ya mtandaoni, andika historia fupi ya Mwalimu Julius Nyerere.

  3. Kumbuka wakati ulipopewa jukumu la kuwasilisha mada fulani. Eleza namna ulivyokusanya taarifa kwa ajili ya uwasilisho huo.

  4. Umepewa kazi mradi kuhusu ujanishaji wa mazingira. Eleza namna vyanzo mbalimbali vya kuaminika vitakavyokusaidia kutekeleza kazi hiyo.

SIFA ZA VYANZO VYA KUAMINIKA VYA TAARIFA ZA KITAALUMA

  • Kuaminika:

    • Sifa za mwandishi

    • Hadhi ya mchapishaji

    • Ushahidi wa mamlaka

  • Usahihi:

    • Ukweli wa maudhui

    • Umakini wa uwasilishaji

    • Data zisizo na makosa

  • Kutopendelea:

    • Maudhui yasiyoegemea upande wowote

    • Uchambuzi wa kitaalamu

    • Hitimisho linalotokana na data

  • Uwazi na Ufasaha:

    • Lugha stahiki kwa hadhira lengwa

    • Uwasilishaji wa hoja kwa uwazi

    • Taarifa sahihi na elekezi

  • Marejeleo:

    • Kunukuu kwa kufuata taratibu rasmi

  • Mpangilio mzuri:

    • Muundo wa kimantiki

    • Vichwa vikuu na vidogo

    • Sehemu ndogo ndogo zenye mtiririko

  • Kusudi na Mawanda:

    • Malengo ya kazi

    • Mawanda ya mada

    • Muktadha wa utafiti

Previous Post Next Post
banner
×

Contact Us