TANGAZO LA KUITWA KAZINI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA 02-05-2026

Mr.Izow
0

Imetolewa rasmi na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 24 Aprili 2025 hadi 17 Machi 2026 kuwa matokeo ya waliofaulu usaili huo yametolewa rasmi.

Tangazo hili linajumuisha majina ya waombaji kazi waliofaulu pamoja na baadhi ya waliokuwa kwenye kanzidata (Database) ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Wasailiwa wote waliofaulu wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal na kupakua barua za kupangiwa vituo vya kazi kupitia sehemu ya My Applications.

Baada ya kupakua barua hizo, wanatakiwa:

  • Kuchapisha (Print) barua za ajira
  • Kuripoti katika kituo walichopangiwa kwa muda uliopangwa
  • Kuwasilisha barua hizo kwa mwajiri husika

Aidha, waombaji wote waliofaulu wanapaswa kufika na vyeti halisi (Original Certificates) kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupewa ajira rasmi.

Kwa wale ambao majina yao hayapo kwenye tangazo hili, tambueni kuwa hawakufaulu au hawakupata nafasi kwa sasa. Hata hivyo, mnahimizwa kuendelea kuomba nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
Pakua au Tazama Orodha Kamili ya Walioitwa Kazini (PDF)
Pata taarifa mpya za ajira kwa haraka zaidi kupitia WhatsApp Channel yetu:

👉 Jiunge hapa

Chapisha Maoni

0 Maoni

Tafadhali Tuambie kupitia hapa

Chapisha Maoni (0)
3/related/default