TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI – HALMASHAURI YA WILAYA YA BARIADI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi kumi na moja (11) baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1. Nafasi na Sifa
Dereva Daraja la II – Nafasi 07
Kazi na Majukumu:- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
- Kufanya usafi wa gari
- Kufanya kazi nyingine kadri utakavyoelekezwa na Mwajiri
- Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV)
- Leseni ya Daraja la C au E
- Uzoefu wa mwaka mmoja wa uendeshaji magari bila ajali
- Mafunzo ya Basic Driving Course (VETA/NIT/Chuo kinachotambuliwa na Serikali)
Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 04
Kazi na Majukumu:- Kuorodhesha barua zinazoingia kwenye regista (incoming correspondence register)
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence register)
- Kusambaza na kupokea majalada kutoka kwa Watendaji
- Kurudisha majalada kwenye reki/kabati la majalada
- Kufuata mzunguko wa majalada (file tracking)
- Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu kulingana na somo husika (Classification & Boxing)
- Kuweka/kupanga kumbukumbu katika reki au mahali panapohifadhiwa
- Kutekeleza kazi nyingine zilizopo chini ya usimamizi wa Msimamizi wake
- Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI)
- Mafunzo ya Diploma (NTA level 6) katika Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
2. Masharti ya Jumla
- Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18–45
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na kutaja ulemavu wao
- Waombaji wambatise CV yenye anuani, namba za simu na majina ya wadhamini watatu
- Waombaji watumishi wa Umma watumie kibali cha waajiri wao kabla ya kuomba
- Vyeti vya Elimu na Taaluma vithibitishwe na Mwanasheria/Wakili
- Testimonial, Provisional Results au Form IV/VI result slips havitakubaliwa
- Waombaji waliostaafu nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na mamlaka husika (TCU, NECTA, NACTE)
- Waajiriwa wa Umma wasio na kibali hawaruhusiwi kuomba
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu hayatafikiriwa
- Muda wa mwisho wa kuwasilisha maombi: 31/03/2026
3. Jinsi ya Kuomba
Maombi yote yafanyike kwa:
- Barua kwa anuani: Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, S.L.P 109, BARIADI
- Au kielektroniki kupitia Ajira Portal
Post a Comment
Tafadhali Tuambie kupitia hapa