Ratiba ya Mitihani ya Diploma ya Ualimu 2026 (DPEE) – Taarifa Rasmi Kutoka NECTA

Mr.Izow
0

Ratiba ya Mitihani ya Diploma ya Ualimu 2026 (DPEE) – Taarifa Rasmi Kutoka NECTA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) imetoa rasmi ratiba ya Mitihani ya Diploma ya Ualimu wa Awali, Msingi na Elimu Maalum (DPEE) kwa mwaka 2026.

Ratiba hii ni muhimu kwa watahiniwa wote kwani inawaongoza kupanga ratiba ya kujisomea na maandalizi yao ya mitihani kwa ufanisi zaidi.

Muhtasari wa Ratiba ya Mitihani

  • Tarehe ya Kuanza: 04 Mei 2026
  • Tarehe ya Kumaliza: 13 Mei 2026
  • Asubuhi: Saa 2:00 – 5:00
  • Jioni: Saa 8:00 – 11:00

Masomo Yatakayofanyiwa Mtihani

  • Elimu na Ujumuishi (Inclusive Education)
  • Mbinu za Kufundishia na Kujifunza
  • Jiografia na Mazingira
  • Kiswahili na Hisabati (Mbinu za Kufundisha)
  • Kiingereza (Mbinu za Kufundisha)
  • Sayansi (Mbinu za Kufundisha)
  • Elimu Maalum

Maelekezo Muhimu

  • Watahiniwa wote wanatakiwa kufika kwenye kituo cha mtihani kwa wakati.
  • Kufuata maelekezo yote yaliyopo kwenye karatasi ya mtihani.
  • Mabadiliko yoyote yatatolewa rasmi na NECTA pekee.
  • Mitihani itaendelea hata siku za sikukuu rasmi.

Ushauri kwa Watahiniwa

Watahiniwa wanashauriwa kuandaa ratiba binafsi ya kujisomea, kupitia mitihani ya zamani na kudumisha nidhamu ya muda. Mafanikio yanategemea maandalizi mazuri na juhudi za kila siku.


Pakua Ratiba Kamili


Kwa taarifa zaidi kuhusu mitihani, matokeo na rasilimali za elimu, endelea kufuatilia Smart Education Tanzania.

Mawasiliano: 0717173853 (WhatsApp / Simu)

Chapisha Maoni

0 Maoni

Tafadhali Tuambie kupitia hapa

Chapisha Maoni (0)
3/related/default