Ajira 630 Mpya Serikalini Zatangazwa 2026: Walimu, Madereva, Makatibu na Kada Nyingine – Tazama Sifa na Jinsi ya Kuomba

Ajira Mpya Serikalini 2026 – Nafasi 630 Zatangazwa Rasmi

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza jumla ya nafasi 630 za ajira kama zilivyoainishwa katika tangazo rasmi.


Nafasi Zilizotangazwa

1. Mwalimu Daraja la III B (Elimu Maalum) – Nafasi 7

Majukumu ya Kazi
  • Kuandaa mipango ya kazi na maandalizi ya masomo
  • Kufundisha, kufanya tathmini na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi
  • Kusimamia mahudhurio ya wanafunzi shuleni na darasani
  • Kutoa malezi, ushauri nasaha na mwongozo wa kitaaluma
  • Kusimamia utunzaji wa vifaa na mali za shule
Sifa za Mwombaji

Cheti cha Kidato cha Nne au Sita pamoja na Stashahada ya Ualimu wa Elimu Maalum kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGTS C


2. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 243

Majukumu ya Kazi
  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri
  • Kupokea wageni na kuwaelekeza
  • Kutunza kumbukumbu za miadi, vikao na ratiba za kazi
  • Kushughulikia majalada na nyaraka za ofisi
  • Kuandaa maandalizi ya vikao na mahitaji ya ofisi
Sifa za Mwombaji

Kidato cha Nne au Sita chenye Stashahada ya Uhazili (NTA Level 6) pamoja na ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi kama Word, Excel, PowerPoint, Internet na E-mail.

Ngazi ya Mshahara: TGS C


3. Daktari wa Mifugo Daraja la II – Nafasi 1

Majukumu ya Kazi
  • Kutoa huduma za afya ya mifugo
  • Kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo
  • Kusimamia udhibiti wa magonjwa ya wanyama
  • Kuratibu ukaguzi wa nyama na machinjio
Sifa za Mwombaji

Shahada ya Veterinary Medicine kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na usajili wa Baraza la Veterinari Tanzania.

Ngazi ya Mshahara: TGS F


4. Mkadiriaji Ujenzi Daraja la II – Nafasi 55

Majukumu ya Kazi
  • Kuandaa BOQ na makisio ya gharama za ujenzi
  • Kuandaa bajeti za miradi
  • Kufanya tathmini na uchambuzi wa miradi ya ujenzi
  • Kusimamia masuala ya fedha za miradi
Sifa za Mwombaji

Shahada au Stashahada ya juu ya Quantity Surveyor kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali pamoja na usajili AQRB.

Ngazi ya Mshahara: TGS E


5. Dereva Daraja la II – Nafasi 296

Majukumu ya Kazi
  • Kukagua gari kabla na baada ya safari
  • Kusafirisha watumishi kwenye safari za kikazi
  • Kufanya matengenezo madogo ya gari
  • Kutunza kumbukumbu za safari
Sifa za Mwombaji

Kidato cha Nne, leseni ya Daraja C au E, uzoefu wa kuendesha gari angalau mwaka mmoja pamoja na mafunzo ya Basic Driving Course kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS B


Nafasi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

  • Mkufunzi Msaidizi Maendeleo ya Jamii II – Food Production (Nafasi 5)
  • Mkufunzi Msaidizi Maendeleo ya Jamii II – Tailoring and Fashion Design (Nafasi 10)
  • Mkufunzi Msaidizi Maendeleo ya Jamii II – Welding and Metal Fabrication (Nafasi 13)

Waombaji wanapaswa kuwa na Stashahada katika fani husika kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS C


Masharti ya Jumla

  • Muombaji awe raia wa Tanzania
  • Umri usiozidi miaka 45
  • Vyeti vyote viwe vimehakikiwa
  • Results slips na testimonials hazitakubaliwa
  • Vyeti vya nje vihalalishwe na TCU, NECTA au NACTVET
  • Uwasilishaji wa taarifa za kughushi utachukuliwa hatua za kisheria

Mwisho wa Kutuma Maombi

04 Aprili 2026


Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa Ajira (Recruitment Portal):

https://portal.ajira.go.tz/

Barua ya maombi ielekezwe kwa:

KATIBU
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P 2320
DODOMA

Post a Comment

Tafadhali Tuambie kupitia hapa

Previous Post Next Post

Featured Post

Smart Education Tanzania