VITUO VYA USAILI WA MAHOJIANO KWA WALIMU NA MKAGUZI WA NDANI DARAJA LA II – FEBRUARI 14, 2026

VITUO VYA USAILI WA MAHOJIANO KWA WALIMU NA MKAGUZI WA NDANI DARAJA LA II – FEBRUARI 14, 2026

Posted on: February 12, 2026

Wasailiwa wote walioteuliwa kufanya usaili wa mahojiano kwa nafasi za:

  • Walimu wa Masomo ya Amali
  • Walimu wa Fizikia
  • Walimu wa Hisabati
  • Mkaguzi wa Ndani Daraja la II (Internal Auditor II)

wanatangaziwa kuwa usaili utafanyika tarehe 14 Februari, 2026.

VITUO VYA USAILI

Wasailiwa wote wanapaswa kuangalia na kuzingatia vituo vya usaili vilivyoainishwa kwenye kiambatisho kilichoambatanishwa hapa chini kulingana na nafasi walizoomba.

MAELEKEZO MUHIMU KWA WASAILIWA

  • Kufika katika kituo walichopangiwa kwa wakati uliobainishwa
  • Kuja na vyeti halisi vya kitaaluma pamoja na nakala zake
  • Kuwa na cheti halisi cha kuzaliwa
  • Kuja na kitambulisho halali cha utambulisho
  • Kuzingatia kikamilifu maelekezo yote yaliyotolewa kwenye tangazo la kuitwa kwenye usaili

Msailiwa atakayeshindwa kuzingatia maelekezo haya hataruhusiwa kushiriki kwenye usaili.



Endelea kufuatilia Smart Education kwa taarifa sahihi za ajira na elimu.

Post a Comment

Tafadhali Tuambie kupitia hapa

Previous Post Next Post

Featured Post

Smart Education Tanzania