Tangazo la Kuitwa Kazini Idara ya Uhamiaji Tanzania – Ratiba ya Usaili Februari 2026

Mr.Izow
0
Uhamiaji Tanzania Logo

Tangazo la Kuitwa Kazini – Idara ya Uhamiaji Tanzania (Februari 2026)

Idara ya Uhamiaji Tanzania chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetangaza rasmi ratiba ya usaili kwa waombaji wa ajira waliotuma maombi kupitia mfumo wa e-Recruitment.

Waombaji wote wanatakiwa kuingia kwenye akaunti zao kupitia tovuti rasmi ya Uhamiaji pamoja na kuangalia barua pepe zao kwa maelekezo ya tarehe, vituo vya usaili na maelekezo muhimu.

Jinsi ya Kuangalia Taarifa za Usaili

Tembelea tovuti rasmi ya Uhamiaji:
www.immigration.go.tz

Vitu Vinavyotakiwa Usailini

  • Namba ya maombi (Application ID)
  • Barua pepe iliyosajiliwa
  • Kitambulisho halali (NIDA, Kura, Passport au kingine rasmi chenye picha)
  • Kalamu ya bluu moja

Mitihani ya Vitendo

Waombaji wa fani zifuatazo watatakiwa kufanya mtihani wa vitendo:

  • Afya
  • Udereva
  • Uhandisi wa mitambo

Tahadhari Muhimu

Kila mwombaji atagharamia mwenyewe usafiri, chakula na malazi wakati wote wa usaili.

Maelezo ya Mawasiliano

Barua pepe: ajira@immigration.go.tz
Tovuti: www.immigration.go.tz

Iliyotolewa na:
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
09 Februari 2026

Pakua Taarifa Kamili (PDF)

BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KAMILI

Endelea kufuatilia Smart Education Tanzania kwa taarifa za ajira, usaili na matokeo mbalimbali nchini.

Chapisha Maoni

0 Maoni

Tafadhali Tuambie kupitia hapa

Chapisha Maoni (0)
3/related/default