Mwongozo Kamili wa Kujaza TASK na SUB TASK za Mwalimu wa Darasani Kwenye ESS (PEPMIS) Portal Tanzania 2026

Mwongozo Kamili wa Kujaza TASK na SUB TASK za Mwalimu wa Darasani Kwenye ESS (PEPMIS)

Mfumo wa ESS/PEPMIS (Employee Self Service – Public Employees Performance Management Information System) unatumika na watumishi wa umma nchini Tanzania kwa ajili ya kupanga, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa majukumu yao ya kazi. Kwa walimu wa darasani, mfumo huu unahitaji kujaza kwa usahihi TASK na SUB TASK kulingana na kazi halisi zinazotekelezwa shuleni.

Makala hii inakupa ufafanuzi sahihi pamoja na PDF tayari itakayokusaidia kujaza taarifa zako kwenye ESS (PEPMIS) bila makosa.


Pakua PDF ya TASK na SUB TASK za Mwalimu wa Darasani

Ili kurahisisha zaidi matumizi ya ESS (PEPMIS), faili la PDF limeandaliwa kwa mpangilio sahihi na linafaa ku-copy au ku-upload moja kwa moja kwenye mfumo.

Pakua PDF Tayari kwa Matumizi ya ESS (PEPMIS)

Baada ya kubofya, faili litaanza kudownload na ukurasa wa matangazo utafunguka kiotomatiki.

DOWNLOAD PDF

1. TASK: KUFANYA MAANDALIZI YA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI

Hii ni TASK ya msingi kwa kila mwalimu wa darasani na inahusisha maandalizi yote muhimu ya kitaaluma.

  • Kuandaa maazimio ya masomo (Schemes of Work).
  • Kuandaa maandalio ya masomo (Lesson Plans).
  • Kufanya majaribio ya kila mwezi na mitihani ya mhula.
  • Kuandaa na kutumia zana za kufundishia na kujifunzia.

2. TASK: KUSHIRIKI MAFUNZO ENDELEVU YA WALIMU KAZINI

  • Kushiriki mafunzo endelevu ya walimu kazini kwa vipindi 39 kwa mwaka.
  • Kuwezesha mada za mafunzo kulingana na ratiba ya vikao vya walimu.

3. TASK: KUSIMAMIA JUKUMU LA MWALIMU SHULENI

Mwalimu anatakiwa kuchagua jukumu moja tu kulingana na cheo au wajibu aliopewa shuleni, kama vile Mwalimu wa Taaluma, Mwalimu wa Nidhamu au Mwalimu wa Malezi na Ushauri.


Hitimisho:
Kujaza TASK na SUB TASK kwa usahihi kwenye ESS (PEPMIS) kunachangia tathmini sahihi ya utendaji kazi wa mwalimu na kuepuka marekebisho yasiyo ya lazima.

Post a Comment

Tafadhali Tuambie kupitia hapa

Previous Post Next Post

Featured Post

Smart Education Tanzania