TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA WALIMU 2026
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) kwa niaba ya MDAs & LGAs anapenda kuwataarifu waombaji wote wa Ajira za Walimu kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 14/02/2026. Waombaji watakaofaulu watapangiwa vituo vya kazi.
MAELEKEZO MUHIMU KWA WASAILIWA
- Usaili utafanyika kwa tarehe, muda na eneo lililotajwa kwa kila kada.
- Kila msailiwa anatakiwa kufika akiwa na kitambulisho halali.
- Msailiwa afike na vyeti halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa hadi shahada.
- Result slips, testimonials au provisional results hazitakubaliwa.
- Vyeti vya nje ya nchi lazima vihalalishwe na TCU/NACTVET/NECTA.
- Kila msailiwa atagharamia usafiri, chakula na malazi.
- Waombaji ambao majina yao hayajaonekana waingie Ajira Portal kuangalia sababu.
PAKUA TANGAZO KAMILI (PDF)
Bonyeza kitufe hapa chini kupakua orodha kamili ya Walioitwa Kwenye Usaili wa Walimu 2026.
Endelea kufuatilia taarifa za ajira na elimu kupitia SmartEducation – www.smarteducation.co.tz

Tafadhali Tuambie kupitia hapa