Mtihani wa Mwezi – Geography Form Two (Februari 2026) | Onicah Secondary School
Pakua Mtihani wa Mwezi wa Geography Kidato cha Pili – Februari 2026 kwa ajili ya mazoezi na maandalizi ya mitihani. Mtihani huu umeandaliwa kwa kuzingatia mtaala wa Tanzania na unasaidia wanafunzi kujipima kabla ya mitihani ya mwisho.
GEOGRAPHY FORM TWO MONTHLY EXAMINATION – FEBRUARY 2026
ONICAH SECONDARY SCHOOL
ONICAH SECONDARY SCHOOL
Pakua Mtihani (PDF)
Maswali ya Mfano Kutoka Mtihani
Swali la 8: Jaza nafasi zilizo wazi
- ________ ni mtikisiko wa ghafla wa ardhi unaosababishwa na nguvu za ndani ya dunia.
- ________ ni mchakato wa kupasuka kwa miamba kutokana na nguvu za tectonic.
- ________ ni kukunjika kwa tabaka za ardhi kutokana na shinikizo la ndani ya dunia.
- ________ ni mwendo wa magma kuelekea au juu ya uso wa dunia.
- ________ ni tabaka la gesi linalozunguka dunia kutokana na mvuto wa dunia.
- ________ ni miamba inayotokana na kupoa na kuganda kwa magma.
- ________ ni mchakato wa mabadiliko ya miamba kutoka aina moja kwenda nyingine kwa muda mrefu.
- ________ ni sehemu ya dunia inayojumuisha crust, mantle na core.
- ________ ni shimo kubwa linalotokea baada ya mlipuko wa volkano kuanguka.
- ________ ni ukuta wa mwamba unaokatiza tabaka za miamba mingine.
Swali la 9
Juma akiwa ndani ya nyumba alihisi mtikisiko mkubwa wa ardhi uliosababishwa na nguvu za asili zinazotokea chini ya uso wa dunia.
- (a) Taja janga lililotokea kwa Juma.
- (b) Taja kifaa kinachopima janga hilo.
- (c) Eleza sababu tatu (3) za janga hilo.
- (d) Eleza athari nne (4) za janga hilo.
Swali la 10 (Sehemu C – Alama 15)
Eleza matokeo matano (5) ya mzunguko wa dunia katika mhimili wake.
Endelea kupata mitihani zaidi, notes na past papers kupitia WhatsApp Channel ya Smart Education .

Tafadhali Tuambie kupitia hapa