TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA MJI BABATI – 2026
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Babati anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi kumi (10) za kazi baada ya kupokea kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Nafasi za Kazi Zilizotangazwa
- Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 6
- Dereva Daraja la II – Nafasi 4
Sifa Kuu kwa Ufupi
- Mwandishi Mwendesha Ofisi II: Awe na Diploma ya Uhazili au NTA Level 6, ajue Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza na matumizi ya kompyuta
- Dereva II: Awe na Kidato cha Nne, Leseni Daraja E au C, na mafunzo ya msingi ya Udereva kutoka chuo kinachotambuliwa
Masharti ya Jumla (Muhtasari)
- Waombaji wawe Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18–45
- Vyeti vyote viwe vimehakikiwa na mamlaka husika
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba
- Maombi yote yawasilishwe kupitia Ajira Portal
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu hayatazingatiwa
Namna ya Kutuma Maombi
Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa Ajira Portal:
https://portal.ajira.go.tz
Tarehe ya Mwisho wa Kutuma Maombi: 16 Januari 2026
Imetolewa na:
Mkurugenzi wa Mji
Halmashauri ya Mji Babati
Post a Comment
Tafadhali Tuambie kupitia hapa