Maswali ya Interview kwa Walimu GRADE IIIA na Majibu
Hapa tumekuandalia maswali 10 muhimu ya interview ikiw ni SET ya Tatu toka tuanze kutoa Maswali haya kwa walimu GRADE IIIA pamoja na majibu yake yenye nguvu. Yanaweza kukusaidia kujiandaa vizuri kabla ya usaili. Tumia link chini ya maswali haya kupakua PDF
1. Eleza maana ya ualimu na wajibu wa mwalimu darasani
Jibu: Ualimu ni kazi ya kitaaluma inayohusisha kufundisha, kulea na kuongoza wanafunzi ili waweze kupata maarifa, stadi na maadili. Wajibu wa mwalimu ni kuhakikisha mazingira ya kujifunzia ni salama, kufundisha kwa mbinu shirikishi, kutathmini maendeleo ya wanafunzi na kuwasaidia wenye changamoto.
2. Ni mbinu zipi shirikishi unaweza kutumia kufundisha darasa la awali au la msingi?
Jibu: Majadiliano, maswali na majibu, uchezaji wa majukumu, vifaa vya kufundishia, kazi za vikundi.
3. Unawezaje kumsaidia mwanafunzi mwenye mahitaji maalum darasani?
Jibu: Kumtambua mapema, kutumia mbinu tofauti kulingana na uwezo wake, kumpa muda wa ziada, kutumia vifaa saidizi, kushirikiana na wazazi na wataalamu.
4. Ni hatua zipi unachukua kudhibiti nidhamu darasani bila kutumia adhabu kali?
Jibu: Kuweka kanuni za darasa, kuwapongeza wanafunzi wanaofuata taratibu, kuwashauri kwa upole wanaokosea, kuwashirikisha katika shughuli za darasa, kujenga uhusiano wa heshima.
5. Unaelewa vipi dhana ya Competence Based Curriculum (CBC)?
Jibu: CBC inalenga kumjengea mwanafunzi maarifa, stadi na mwelekeo wa kimaadili ili aweze kutumia ujuzi huo katika maisha ya kila siku. Inasisitiza kujifunza kwa vitendo, ushirikishwaji wa wanafunzi, na utathmini endelevu.
6. Kwa nini unataka kuwa mwalimu wa GRADE IIIA?
Jibu: Kwa sababu napenda kufundisha na kuchangia katika maendeleo ya watoto wa Tanzania. Nafasi hii itanipa uwezo wa kutumia taaluma yangu kuandaa kizazi chenye maarifa, stadi na maadili bora.
7. Ungeandaa vipi somo la hesabu kwa darasa la IIIA ili liwe rahisi kueleweka?
Jibu: Kuhusisha hesabu na maisha ya kila siku, kutumia vifaa vya kufundishia, kuandaa maswali ya vitendo, kuruhusu wanafunzi kushirikiana kwa vikundi.
8. Eleza nafasi ya mwalimu katika malezi ya kijamii na kimaadili
Jibu: Mwalimu ni kioo cha jamii, hufundisha maadili, husaidia wanafunzi kujenga tabia njema, na kuwaongoza kuwa raia wenye uwajibikaji.
9. Ni changamoto zipi mwalimu anakutana nazo darasani na namna ya kuzitatua?
Jibu: Changamoto ni pamoja na upungufu wa vifaa, tofauti za uwezo wa wanafunzi, na nidhamu. Suluhisho ni ubunifu, kutumia mbinu shirikishi, na kushirikiana na wazazi.
10. Eleza umuhimu wa tathmini endelevu kwa wanafunzi
Jibu: Tathmini endelevu husaidia kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi, kubaini changamoto mapema, na kutoa mrejesho wa mara kwa mara ili kuboresha ujifunzaji.
© SmartEducation.co.Tz

