Call for Oral Interview at Mahakama December 2025
Judicial Service Commission (JSC) inawaarifu waombaji wote wa ajira mbalimbali kuwa, baada ya kukamilika kwa usaili wa hatua ya kwanza (First Stage Interviews) uliofanyika kuanzia tarehe 16 Desemba hadi 23 Desemba, 2025 katika vituo mbalimbali nchini, majina ya waombaji waliofanikiwa kuchaguliwa kuendelea na hatua ya pili ya usaili (Oral Interview) yametangazwa rasmi.
Hatua ya Pili: Oral Interview
Waombaji ambao majina yao yanaonekana kwenye tangazo hili wamechaguliwa kushiriki usaili wa mdomo (Oral Interview). Tarehe pamoja na vituo vya usaili vimeainishwa kwenye orodha ya waombaji walioteuliwa (Shortlisted Candidates List).
Tahadhari Muhimu kwa Kada Maalum
Waombaji wa nafasi zifuatazo:
- Office Assistant II (Mwandishi Mwendesha Ofisi II)
- Driver II
Watatakiwa kwanza kufanya Practical Interview. Ni waombaji watakaofaulu usaili wa vitendo pekee ndio watakaoruhusiwa kuendelea na usaili wa mdomo (Oral Interview).
Ratiba ya Usaili
- Tarehe za Usaili: 5 Januari hadi 16 Januari, 2026
- Muda wa Kuripoti: Saa 2:00 asubuhi (8:00 A.M.)
Nyaraka Muhimu za Kuja Nazo
Waombaji wote waliochaguliwa wanatakiwa kufika wakiwa na nakala halisi (Original Copies) za nyaraka zifuatazo:
- Vyeti vya Taaluma (Academic Certificates)
- Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificates)
- Cheti cha Kuzaliwa
- Kitambulisho kimoja halali cha Serikali chenye picha, kama:
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Kitambulisho cha Mpiga Kura
- Pasipoti
- Leseni ya Udereva
Masharti Muhimu
- Waombaji watakaoshindwa kuwasilisha nyaraka zote hawatafanyiwa usaili
- Waombaji watakaofika nje ya muda uliopangwa hawataruhusiwa kufanya usaili
- Kila mwombaji anatakiwa kuhudhuria usaili katika kituo alichopangiwa pekee
Waombaji ambao majina yao hayapo kwenye orodha ya walioteuliwa wanapaswa kufahamu kuwa hawakufanikiwa kuendelea na hatua ya pili ya usaili.
Download PDF ya Majina ya Waliochaguliwa
Bofya kitufe hapa chini kupakua PDF yenye orodha ya waombaji waliochaguliwa kushiriki usaili wa Oral Interview Mahakama:
Taarifa Zaidi
Kwa taarifa kamili na matamko rasmi, tembelea tovuti ya Judicial Service Commission:
www.jsc.go.tz
Mawasiliano
Kwa maswali au ufafanuzi zaidi, wasiliana nasi masaa 24 kupitia:
Simu: 0734 219 821 / 0738 247 341
Barua pepe: maulizo.ajira@jsc.go.tz
AjiraPort | Smart Education
Chanzo chako cha taarifa sahihi na za haraka kuhusu Ajira, Usaili
na Fursa za Kazi Tanzania.
