Nafasi za Kazi za Kuhamia Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) 2026 – Serikali ya Tanzania

Nafasi za Kazi za Kuhamia Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) 2026

Ofisi ya Msajili wa Hazina (Office of the Treasury Registrar – OTR) imetangaza nafasi za kazi za kuhamia (transfer) kwa watumishi wa umma wenye sifa stahiki kwa mwaka 2026.

Nafasi hizi zinalenga watumishi wa umma wanaokidhi vigezo vilivyowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

GENERAL CONDITIONS

  1. Waombaji wote lazima wawe waajiriwa wa Serikali (Public Service).
  2. Waombaji wanapaswa kuomba kwa kuzingatia taarifa zote zilizotolewa kwenye tangazo hili.
  3. Waombaji lazima waambatanishe nakala zilizothibitishwa (certified copies) za vyeti vifuatavyo:
    • Postgraduate / Degree / Advanced Diploma / Diploma / Certificates
    • Transcripts za Postgraduate / Degree / Advanced Diploma / Diploma
    • Vyeti vya Usajili wa Kitaaluma na Mafunzo kutoka Mamlaka husika (ikiwa inahitajika)
    • Cheti cha Kuzaliwa
  4. Hairuhusiwi kuambatanisha nakala za: Form IV na Form VI results slips, Testimonials, au transcripts zisizokamilika.
  5. Muombaji lazima apakie Passport Size Photo ya hivi karibuni kwenye Recruitment Portal.
  6. Mtumishi aliyestaafu katika Utumishi wa Umma kwa sababu yoyote haruhusiwi kuomba.
  7. Muombaji anatakiwa kuonyesha marejeo (referees) watatu wanaoaminika pamoja na mawasiliano yao sahihi.
  8. Vyeti vyote vya masomo vilivyopatikana nje ya Tanzania lazima vitambuliwe na mamlaka husika (TCU, NECTA, NACTVET). Waombaji wa nafasi zenye hitaji la GPA lazima waambatanishe cheti cha mahesabu ya GPA kutoka TCU.
  9. Barua ya maombi iliyosainiwa iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza na ipelekwe kwa:

    Secretary,
    President’s Office,
    Public Service Recruitment Secretariat,
    P.O. Box 2320,
    Mahakama Street, Tambukareli,
    Dodoma.
  10. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 11 Februari, 2026.
  11. Ni waombaji watakaofikia hatua ya usaili pekee watakaopata taarifa.
  12. Kuwasilisha vyeti vya kughushi au taarifa za uongo kutachukuliwa hatua za kisheria.

Smart Education itaendelea kukuletea matangazo rasmi ya ajira za Serikali, nafasi za kuhamia kazini, internships, na fursa nyingine muhimu Tanzania.

Post a Comment

Tafadhali Tuambie kupitia hapa

Previous Post Next Post

Featured Post

Smart Education Tanzania