Ajira Mpya Gairo 2026 | Nafasi 7 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

Ajira Mpya Gairo 2026 | Nafasi 7 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI – HALMASHAURI YA WILAYA YA GAIRO

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi saba (7) katika Halmashauri hiyo, baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 02

1.1 Majukumu na Kazi

  • Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka kwenye rejista husika
  • Kusambaza na kupokea majalada kutoka kwa watendaji
  • Kutafuta kumbukumbu, nyaraka na majalada yanayohitajika
  • Kurudisha majalada kwenye kabati au sehemu husika za kuhifadhia
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi
  • Kutekeleza majukumu mengine ya fani atakayopangiwa

1.2 Sifa za Mwombaji

Mwombaji awe amehitimu Kidato cha Nne au Sita (Form IV / VI) na awe na Stashahada au NTA Level 6 ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, pamoja na ujuzi wa kutumia Kompyuta.

1.3 Ngazi ya Mshahara

TGS C


2.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 05

2.1 Majukumu na Kazi

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari
  • Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi
  • Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari
  • Kufanya usafi wa gari
  • Kutekeleza majukumu mengine ya fani atakayopangiwa

2.2 Sifa za Mwombaji

Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C, awe amefanya kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali, na awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.

2.3 Ngazi ya Mshahara

TGS B


3.0 Masharti ya Jumla

  1. Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18–45
  2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba
  3. Cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa kiambatishwe
  4. Maombi yaambatane na CV yenye waamuzi (referees) watatu
  5. Vyeti vyote viwe vimehakikiwa kisheria
  6. Matokeo ya muda (results slips) hayatazingatiwa
  7. Waombaji wawe na NIDA au Namba ya NIDA
  8. Tofauti za majina au herufi zifafanuliwe kwa hati husika
  9. Waombaji waliowahi kutiwa hatiani hawaruhusiwi
  10. Waajiriwa wa Serikali wasio kwenye nafasi za kuingilia wasiombe
  11. Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria

Namna ya Kutuma Maombi

Maombi yote yatumwe kupitia Ajira Recruitment Portal:
https://portal.ajira.go.tz/

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 17 Januari, 2026.

Anuani ya barua:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo,
S. L. P 40,
Gairo.


Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

Post a Comment

Tafadhali Tuambie kupitia hapa

Previous Post Next Post

Featured Post

Smart Education Tanzania